Jumatano, 4 Novemba 2015

Alan Wanga kaeleza experience

 ya maisha ya Sudan,

 ukinywa pombe hii ndio adhabu

 utakayopewa........


Mshambuliaji wa kimataifa wa Kenya anayekipiga katika klabu ya Azam FC ya TanzaniaAlan Wanga November 4 amefunguka katika kituo kimoja cha radio Tanzania kuhusu maisha yaSudan, nchi ambayo utamaduni wake ni tofauti na nchi nyingi za Afrika Mashariki kamaKenyaTanzania na Uganda.
Awali tuliwahi kusikia stori kuhusu nchi ya Sudan ambayo sheria zake ni ngumu na utamaduni wake tofauti na utamaduni wa nchi za Afrika MasharikiAlan Wangaamejiunga msimu huu na Azam FC akitokea Al-Merreikh ambayo alidumu nayo katika kipindi cha mwaka mmoja, awali tuliwahi kusikia kuwa Sudan ukinywa pombe ni kosa kisheria? Wanga ana majibu haya.
Allan-Wanga
“Ni kweli kuna sheria ngumu kule kama wewe ni mchezaji ambaye hauna malengo na hujui kazi yako itakuwa vigumu sana kuishi, kule hakuna klabu za usiku wala Bar kwa wale wachezaji ambao ndio wanaanza soka Sudan ni mahali pagumu kuishi, Sudan ukipatikana na pombe au umelewa nadhani sheria yao ni kupigwa viboko 40 na kama wewe ni raia wa kigeni unaweza rudishwa nchini kwenu” >>> Alan Wanga
Kama utakuwa unakumbuka vizuri Alan Wanga ni mshambuliaji ambaye alienda Petro Atletico ya Angola kurithi nafasi ya Manucho ambaye alijiunga na Man United yaUingereza mwaka 2008, Wanga pia amewahi kucheza klabu ya FK Baku ya Azerbaij.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni