ENTERTAINMENT
Billboard imetoa list ya rappers
wakali duniani… lakini
Snoop Dogg ameichukuliaje
list hiyo!?

Baada ya mtandao wa Billboard kuachia orodha yao ya 10 Greatest Rappers Of All Time, kumekuwa na maneno mengi sana kwenye mitandao ya kijami kuhusu 2 Pac, Kanye West na Drake kutokutajwa kwenye orodha hiyo.
Billboard hawakukaa kimya, walitoa sababu za kwanini watu kama Kanye West na 2 Pachawakuepo kwenye orodha hiyo, sababu kubwa iliyogusiwa ni kwamba vigezo viliyotumika ni kuangalia nani ni MC bora zaidi na sio nani ni msanii bora zaidi!
Lakini kuna baadhi ya watu bado wanadai kuwa kutemwa kwa 2 Pac kwenye orodha hiyo ni kitendo kinachoshusha heshima ya muziki wa HipHop Marekani na mmoja ya wasanii hao ni Snoop Dogg!
Snoop Dogg kaamua kusema yake kupitia page yake ya Instagram kwa kupost picha ya orodha hiyo na caption ya maneno inayosema…
>>>”This is so disrespectful. !!” the Long Beach, California rapper writes under an image of Billboard’s list. “Whoever did this list need a swift kick in the A**. No. Tupac. Come on cuz ?. Jus my opinion.” <<< Snoop Dogg.
Je, wewe unaonaje mtu wangu? ni sahihi kwa Billboard kutokumtaja 2 Pac kama miongoni ya rappers/ Mc’s 10 bora wa duniani!? Ni kweli 2 Pac hakuwa MC mkali?



Hakuna maoni:
Chapisha Maoni