Jumatatu, 9 Novemba 2015

ENTERTAINMENT

Hapa ni Christian Bella 

pembeni mkongwe 

Koffi Olomide

 ndani ya studio.. Kitu kipya?

Kama umekuwa karibu na mtandao wa Instagram utakuwa umeshuhudia mastaa wengi wakipost vipande vya video ya wimbo mpya wa Koffi Olomide unaoitwa ‘Selfie’.
Koffi ni mkongwe wa muziki toka Congo, ni moja ya majina machache yaliyodumu kwenye muziki long time sana… Hakuna mwenye wasiwasi kuhusu ubora na ukali waChristian Bella inapokuja kwenye suala la muziki wake.
Kuna picha amepost Christian Bella kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa na Koffindani ya studio halafu caption inasomeka hivi >>>> ‘Nikiwa studio na big artist @koffiolomide_officiel .. Kazi nzuri inakuja‘>>> @bellachristian1
Hiyo ni dalili nzuri kwamba collabo ya Koffi Olomide na Christian Bella ndio story nyingine kubwa inayokuja any time kuteka vichwa vya habari za burudani.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni