Alhamisi, 5 Novemba 2015

Iyobo: Nani Anasema Aunt Mzee?

Iyobo: Nani Anasema Aunt Mzee?
     

    Kafunguka! Dansa wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambaye ni mwandani wa staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson, Moses Iyobo amewatolea uvivu baadhi ya watu wanaomsema Aunt kuwa ni mzee kwa kuwa amempita umri, jambo ambalo hakubaliani nalo.
    Akizungumza na mwanahabari wetu, Iyobo alitiririka kuwa anawashangaza watu wanaoingilia mapenzi yao kwani yeye anachojua kwenye mapenzi watu hawaangalii umri ila ni upendo na kuheshimiana.
    “Nani anasema Aunt ni mzee? Mimi namuona ni mtoto mbichi kabisa,” alisema Iyobo mwenye umri wa miaka 23 huku Aunt akiwa na 29.

    Hakuna maoni:

    Chapisha Maoni