Karim Benzema afikishwa
mahakamani kisa mkanda
wa ngono, hizi ni picha zake
akiwa mahakamani…

Mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa anayekipiga katika klabu
ya Real Madrid yaHispania Karim Benzema amezidi kuingia katika headlines
baada ya zile stori za kuvuja kwa kanda ya ngono kuendelea kuchukua nafasi,
Jumatano ya November 4 Benzemaaliripotiwa kukamatwa kwa kosa hilo ila leo
November 5 amefikishwa mahakamani.
Staa huyo wa Real Madrid aliyekuwa akihusishwa kuhamia katika klabu ya Arsenal yaUingereza katika dirisha la usajili lililofungwa mwezi August 2015 ameingia katika kashfa hiyo pamoja na rafiki yake wa utotoni ambaye anacheza naye katika timu ya taifa yaUfaransa Mathieu Valbuena.
Mshambuliaji huyo inatajwa katozwa faini sambamba na kufungiwa
kuonana na mchezaji mwenzake wa ufaransa, hata hivyo ripoti ya
kichunguzi kutoka Ufaransa zinasema kosa alilolifanya Benzema lingeweza
kumfanya afungwe jela miaka mitano ila taarifa kutoka kwa
mwanasheria wa staa huyo Sylvain Cormier ameviambia vyombo vya habari
kuwa mteja wake hana hatia.
Benzema aliyekuwa anasumbuliwa na majeruhi na Mathieu Valbuena waliachwa
katika kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa mapema mwezi huu. Benzema
kwa sasa anatoka na Analicia Chaves ambaye alikuwa
mpenzi wa staa wa soka wa Ubelgiji Axel Witsellakini aliwahi kuhusishwa
kutoka na msanii wa pop kutoka Marekani Rihanna.





Hakuna maoni:
Chapisha Maoni