Jumatatu, 9 Novemba 2015

MICHEZO

Ivo Mapunda amejiunga na

Azam FC? hizi ni sentensi za

 majibu yake…

Golikipa mkongwe Tanzania aliyewahi kuvichezea vilabu vya Dar Es Salaam Young African na Simba Ivo Mapunda amethibitisha kuwa na mpango wa kujiunga na moja kati ya klabu zilizokuwa zinamnyatia kwa muda mrefu. Ivo Mapunda ambaye kwa sasa hana timu amethibitisha kuwa na mpango wa kwenda kujiunga AFC Leopards ya Kenya.
Ivo Mapunda ambaye alikuwa amekaa bila kuwa na timu kwa miezi kadhaa baada ya kuachwa na Simba kutokana na madai ya viongozi wa Simba kusema kuwa Ivo alikuwa anakwepa kusaini mkataba licha ya kuwa alikuwa amepewa tayari fedha za usajili, hivi karibuni amekuwa akihusishwa kujiunga na Azam FC ambayo anafanya nayo mazoezi.
mapunda-dive
“Kiukweli nimeomba kufanya mazoezi Azam FC inawezekana mafanikio yangu mimi yakawa yanatokana na wao kunikaribisha kufanya mazoezi na kulinda kipaji changu, kwa hiyo mipango ya kwenda Kenya ipo muda wowote kuanzia hivi sasa naweza kwenda Kenya Ligi kule imeisha, kuhusu kujiunga Azam FC hizo ni tetesi ambazo hata mimi nazipata magzetini ila sijaambiwa chochocte na Azam nilichokifanya Azam nikuomba kufanya mazoezi”>>> Ivo
Golikipa huyo ambaye anapenda kutundika taulo jeupe akiwa golini amethibitisha kuwepo na mazungumzo ya yeye kurudi Kenya kujiunga na AFC Leopards baada ya Ligi yaKenya kumalizika, hii itakuwa sio mara ya kwanza kwa Ivo kwenda kucheza soka Kenyakwani amewahi kucheza vilabu vya Bandari na Gor Mahia vyote vya nchini humo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni