Nimeamua Kumwimbia Mungu- Matumaini
WASWAHILI husema kabla ya kufa haujambika, inawezekana neno hilo utokana na madhira yamkutayo mtu msanii komediani wa Kike Tumaini Martin ‘Matumaini’ anasema kuwa baada ya kuugua amemtolea Bwana maisha yake ameokoka na anaimba nyimbo za Injili.
“Namshukru Mungu kwa mapito niliyopitia, nimeamua kumkabidhi Mungu maisha yangu kwa kumuimbia na wimbo wangu wa kwanaza ulikuwa ni Nimepona nikimshukru Mungu kwa muujiza wake,”anasema Matumaini.
Matumaini anasema kuwa ana albanu ya nyimbo sita ambazo zote amemshirikisha pacha wake katika fani ya uchekeshaji Kiwewe na wanaimba kikomediani kama wafanyavyo katika Komedi zao, Matumaini anasali katika kanisa la Mito ya Baraka.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni