Jumamosi, 21 Novemba 2015

Rais Magufuli alivyoagiza 

mil. 200 za sherehe ya Wabunge

zipelekwe Muhimbili.. 


Hii stori ilianza kuenea kwenye mitandao ya kijamii, wapo walioamini na wapo walioona kama huo ni ujumbe wa uzushi… wakati unavyozidi kusogea ukweli umezidi kuthibitika kwamba haikuwa uzushi, agizo hilo limetolewa na Rais Magufuli mwenyewe !!
Nakusogezea uthibitisho mwingine kutoka Ikulu, hii ni nukuu ya alichokisema Rais Magufuli kuhusu agizo hilo >>> “Nitaomba mnisamehe sana, inawezekana sherehe ya leo isiwe nzuri kama mlivyozoea, hakuna bia… inawezekana kama kuna chupa za wine ni chache, mengi ni mani na soda.”
Sentensi zake nyingine hizi hapa >>> “Nilipoambiwa kwamba zimechangwa shilingi milioni 250 kwa ajili ya sherehe, nikasema fedha hizo zipelekwe katika hospitali ya Taifa Muhimbili zikasaidie kununua vitanda“- Dk. J.P Magufuli


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni