Alhamisi, 5 Novemba 2015

SIASA

Nimethibitishiwa kuhusu 

Dk. Magufuli kufanya uteuzi 

wa Mwanasheria Mkuu TZ.. 


Ni saa chache tu zimepita toka Rais wa awamu ya tano, Dk. John Pombe Magufuliaapishwe 

na kuanza kazi yake kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na Makamu wake, 

Mama Samia Suluhu Hassan… mpya nyingine ni juu ya uteuzi wa Mwanasheria Mkuu anayeanza majukumu

 yake mapya kwenye Serikali ya tano inayoongozwa na ‘Tingatinga Magufuli

Masaju
Kazi imeanza, Rais Magufuli amemteua George Mcheche Masaju kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na kesho November 06 2015 ataapishwa Ikulu Dar es Salaam.
Mwanasheria huyo sio mgeni kwenye nafasi hiyo, George Masaju alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali iliyomaliza muda wake iliyoongozwa na Rais Mstaafu Jakaya Kikweteambapo aliishika nafasi hiyo baada ya aliyekuwa anaongoza wakati huo, Jaji Frederick Werema kujiuzulu December 2014 wakati wa sakata la ESCROW.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni