Jumanne, 1 Desemba 2015

ENTERTAINMENT

Kuna uwezekano wa Will Smith

kuingia kwenye Siasa? 

Hii ndio mipango yake 

ya badaaye…

Mkali wa kuigiza movie kutoka HollywoodWill Smith anafahamika kama mmoja ya wasanii wakubwa sana duniani, ukiachia hayo Will Smith amejijengia jina kubwa sana kwenye muziki kama rapper lakini nini kinaendelea kichwani mwa staa huyo kuhusu maisha yake ya badaaye?
Nimekutana na interview aliyofanya Will Smith na The Hollywood Reporter siku chache zilizopita na humo Will amegusia ndoto za kuingia kwenye siasa miaka ya karibuni.
SMITH2
>>> “Sipendi kukaa sehemu moja kwa muda mrefu, kwahiyo nahisi mpaka hapa nilipofikia naendelea kukuza uwezo wangu wa kutoa mchango wangu duniani… nimepitia vitu vingi kwenye kila kitu nilichokigusa kwenye safari yangu na inafika wakati unaona inabidi uendelee kuiandika stori yako kwa kuangalia majukwaa mengine yanayoweza kutoa kile kilicho ndani yako na kushare na wengine… nikilitazama dirisha la siasa naona kuna uwezekano wa mimi kuwa na future nzuri tu huko. Wanaweza wakanihitaji siku moja kutumia sauti yangu na mawazo niliyonayo…” <<< Will Smith.
FRANKFURT AM MAIN, GERMANY - FEBRUARY 01:  Arnold Schwarzennegger, actor and former Governor of Califonia, attends the Lloyd Cleantech Congress on February 1, 2013 in Frankfurt am Main, Germany. The Thomas Lloyd Group invited Investors and guests to discuss actual technologies and trends in renewable energies.  (Photo by Hannelore Foerster/Getty Images)
Ikiwa kama mipango hii itafanikiwa, Will Smith atakuwa staa wa pili wa movie zaHollywood kujiunga na Siasa baada ya mkali wa movie za Action, Marekani, Arnold Schwarzenegger kuweka nguvu yake kubwa kwenye sekta hiyo miaka zaidi ya mitano iliyopita ambaye kwenye safari yake ya kisiasa alishawahi kuwa Gavana wa Califonia.
SMITH3
Kwa sasa Will Smith anakamilisha movie yake mpya iitwayo ‘Concussion’ movie ambayo Will anacheza kama daktari wa KinigeriaDr. Bennet Omalu. Movie hiyo itakuwa mtaani kuanzia tarehe 25 December 2015.
Itazame Trailer yake hapa chini kwenye hii video:

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni