Alhamisi, 29 Januari 2015

GOOD NEWS FROM DVJ LUDY B:Haya ni ya Davido kuhusu nafasi ya Urais Nigeria…
Tumeona baadhi ya mastaa wakijiingiza katika ushu za kisiasa, wengine wawanafanikiwa kushika nafasi mbalimbali za uongozi na kufanya vizuri, lakini wapo ambao ndoto zo hazitimii pia.
Nakusogezea hii kutoka Nigeria, wao wanakaribia kufanya uchaguzi mkuu na maandalizi ya kampeni yameanza, mengi yameendelea huku wengine wakiachia nyimbo za kushawishi watu kujitokeza na kuchagua viongozi bora kwa maslagi ya wote.
Kituo cha MTV Base kinafanya kampeni za kuhamasisha vijana kupiga kura kwa busara katika uchaguzi mkuu ujao, miongoni mwa vijana walioko kwenye video za kampeni hiyo ni pamoja na mastar kama 2Face Idibia, Banky W, Ebuka, Sound Sultan, Emmanuel Ikubese, Davido, Reminisce, Yemi Alade na wengineo.
Maneno ya Star Davido katika kampeni hiyo iliyopewa jina la ‘Choose Or Lose’ baada ya kuulizwa swali kama angepewa nafasi ya kumchagua star yoyote wa Naija kuwa Rais angemchagua nani?
Davido akasema anaona kama yeye anafaa zaidi na atakachokifanya ni kutengeneza barabara zilizoharibika na vitu vingine, ndani ya miaka 10 anaamini nchi hiyo itakuwa katika hali ya usafi pamoja na  majengo ya kifahari.
“Yes! I’m voting, I want my voice to be heard, there’s no point in complaining if you are not going to vote“– Davido.
“I think I’m good enough to be president, because it’s me, I want to be the president“– Davido.
Bonyeza play kumsikiliza Davido akizungumzia ishu hiyo.https://www.youtube.com/watch?v=dNhNvrPoh14

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni