Alhamisi, 26 Novemba 2015

ENTERTAINMENT

Kitu kipya cha Jamie Foxx, 

‘In Love By Now’ kipo hewani 

tayari na video yake 

imenifikia! – (Video).

Staa wa movie Hollywood, Marekani na msanii wa R&B, Jamie Foxx anaziandika headlines za leo kwenye kurasa za burudani na ujio wa single mpya inayopatikana kwenye latest Album yake, Hollywood: A Story of a Dozen Roses.
Wimbo unaitwa ‘In Love By Now’ na official music video yake ipo hewani tayari… video queen wa single hii ni Nicole Scherzinger mmoja ya wasanii waliokuwa wanaunda kundi la muziki la Pussycat Dolls, Marekani… Nicole ambaye amecheza kama mke mtarajiwa wa Jamie Foxx anafanya maamuzi ya kumuacha Foxx katikati ya umati wa watu kanisani, licha ya Jamie Foxx kujaribu kumuwahi jitihada zake zinakwama njiani.
JAMIE3
Unaweza ukacheki muendelezo wa stori nzima kati ya wawili hao kwenye video hii ya dakika nne hapa chini.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni