Good News kwa familia ya
mchekeshaji Eddie Murphy,
ni huu ugeni mwingine!!
Mchekeshaji maarufu duniani Eddie Murphy ameingia kwenye headlines baada ya kutangaza anatarajia ugeni ndani ya familia yake.
Staa huyo pamoja na mchumba wake Paige Butcher wanatarajia kupata mtoto ambaye atakua wa kwanza ndani ya uhusiano wao lakini akiwa ni mtoto wa tisa kwa mchekeshaji huyo.
Wawili hao wamedumu kwenye uhusiano kwa miaka mitatu na wanatarajia kupata ugeni huo May, 2016.
Eddie ana watoto watano na mke wake waliyetengana 2006 baada ya miaka 22 ya ndoa yao Nicole Murphy, pia alizaa mtoto mmoja na aliyekuwa mpenzi wake Paulette McNeely, pia mtoto mwingine alizaa na Tamara Hood pamoja na Angel Iris.
Eddie Murphy about to have kid number 9 and Baby’s Mama number 5.
— Twice Sifted (@twice_sifted) November 5, 2015


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni