Hakitupwi kitu hapa !!…
zile chupa unaziona takataka,
Nigeria wamejengea mpaka
nyumba.. (+Pichaz)

Maisha yanabadilika kila siku, zamani ilikuwa ukikutana na chupa au makopo ya maji au juice unayaona takataka… sasahivi ni dili na watu wameweka nguvu zao kabisa kukusanya makopo na kuyauza !!
Nigeria wamefanya kitu kingine zaidi mtu wangu, umewahi kuona nyumba za makopo??!! Nigeria wamefanya kitu hicho, wamejenga nyumba kwa makopo ambapo ndani ya makopo hayo kumejazwa mchanga halafu makopo yanapangwa vizuri kabisa mpaka inakuwa nyumba ya kuishi.
Sifa nyingine kubwa za hizi nyumba ni kwamba zina uwezo wa kuzuia risasi na pia zinaweza kuzuia moto.
Unaweza kuwa na swali kwamba chupa kiasi gani au chupa ngapi zinatosha kukamilisha mjengo??!! Jibu lake ni hili hapa, kama unahitaji nyumba ya vyumba viwili inatakiwa kuwepo na chupa 14,000… Umevutiwa na ujenzi wa aina hii mtu wangu ???






Hakuna maoni:
Chapisha Maoni