Jumanne, 3 Novemba 2015

Utapenda kuiona behind the scenes ya video mpya ya Tinashe; ‘Player’ feat. Chris Brown – (Video)!

Wakati tukiwa tunaendelea kuisubiri official music video ya Player ya kwake Tinashe featChris Brown, msanii huyo mwenye miaka 22 ameona itakuwa poa zaidi kama akiisogeza kwetu behind the scene ya video hiyo kwa sasa.
Single ya Player inapatikana kwenye Album mpya ya Tinashe iliyopewa jina ‘Joyride’, kizuri zaidi kuhusu single hii ni kwamba wimbo huu umeandikwa na rapper Travi$ Scottambaye pia ameshirikishwa kwenye baadhi ya nyimbo kwenye album hii mpya.
NASHE2
Hii itakuwa Album ya pili ya Tinashe toka aanze muziki, Album yake ya kwanza ilitoka mwaka 2014 na ilipewa jina la Aquarius ambapo kutoka kwenye album hiyo tuliweza kusikia nyimbo kama 2 On, All Hands on Deck, na Pretend.
NASHE3
Tinashe anategemea kuzindua album yake mpya mwishoni wa mwaka 2015… ila hapa chini nimekusogezea video ya behind the scene ya wimbo wake mpya; Player (feat Chris Brown).

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni