Jumatano, 2 Desemba 2015

ENTERTAINMENT

Wasanii waliosikilizwa zaidi

kwa 2015 watajwa, Drake,

Rihanna na Fetty Wap 

wamo pia!

Mwaka wa 2015 umekuwa mwaka poa sana kwa rapper anaeunda kundi la Young Money, Drizzy Drake… baada ya kuisuka list ya Hot 100 Beatles kwa kuibuka kwenye nafasi ya juu zaidi, mafanikio ya rapper huyo yanazidi kuweka headlines baada ya mtandao wa Spotify kumtaja Drake kama ‘most streamed artist of the year‘.
spot4
Drake.
Kwa mujibu wa mtandao wa Billboard na Spotify wenyewe, kwa mwaka huu wa 2015,Drake amekuwa msanii pekee aliyesikilizwa na watu zaidi ya mara bilion 1.8 mtandaoni na wasikiliaji milion 46!
spot2
Rihanna.
Latest hitsong yake Hotline Bling, mixtape yake ya If You’re Reading This It’s Too Latepamoja na mixtape ya pamoja aliyofanya na Future; What A Time to Be Alive ndio kazi zilizoongza kwa kusikilizwa zaidi mtandaoni… kwa upande wa wanawake Pop Staa,Rihanna ndio msanii wa kike aliyeongoza kwa kusikilizwa zaidi kwa mwaka 2015 akiwa amesikilizwa zaidi ya mara bilion 1.
Spot3
Fetty Wap.
Album ya Drake; If You’re Reading This It’s Too Late inashika nafasi ya Album inayosikilizwa zaidi mitandaoni kwa Marekani na wimbo wa Fetty Wap ‘Trap Queen’unaongoza chati kama wimbo unaosikilizwa zaidi kwenye mitandao.
Billboard imeendelea kuwataja wasanii tano bora kutoka Marekani wanaoongoza kwa kusikilizwa zaidi mitandaoni na wasanii hao ni:
  1. Drake
  2. The Weekend
  3. Kanye West
  4. Ed Sheeran
  5. Eminem.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni