MICHEZO
Cristiano Ronaldo
kazindua movie yake London,
Ferguson, Mourinho na
Ancelotti ndani
(+Pichaz&Video)

Mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno anayekipiga katika klabu ya Real Madrid yaHispania Cristiano Ronaldo usiku wa November 9 alifanya uzinduzi rasmi wa movie yake ambayo anataja kuiandaa kwa ajili ya mashabiki wake, Ronaldo kafanya uzinduzi movie yake inayoitwa ‘Ronaldo’ akiwa pamoja na mama yake na mtoto wakeCristiano Ronaldo Junior.
Uzinduzi huo uliyofanywa Leicester Square katika jiji la London Uingereza ulihudhuriwa na makocha wa zamani wa staa huyo ambao ni Sir Alex Ferguson, Jose Mourinhona Carlo Ancelotti sambamba na uwepo wa wakala wake Jorges Mendes na mastaa wengine wengi.

Ronaldo akiwa na kocha wake wa zamani wa Man United Sir Alex Ferguson aliyekuwepo katika uzinduzi huo.
Movie hiyo ambayo imechezwa kwa zaidi ya miezi 14 kwa asilimia kubwa inahusisha maisha halisi ya staa huyo ambaye alianzia maisha yake soka katika klabu ya Sporting Lisbon ya kwa Ureno, Ronaldo amefanya uzinduzi huo sambamba na kufanya interview fupi katika red carpet.
“Wakati nilipowasiliana na watu kutokaUniversal kuhusu movie walipanga kufanya movie hii kwa siku kama tatu, ila najisikia vizuri kufanya kazi na director Anthony na Paul, katika movie hiyo utapata nafasi ya kuona vitu vyangu vingi binafsi na nimefurahia kufanya movie, nafikiria itakuwa na mrejesho mzuri kwangu ila kwa watu wanaonifahamu hawatoshangazwa na hii, ila mimi nimefanya kwa ajili ya mashabiki ambao wamekuwa na mimi katika shida na raha”>>> Ronaldo








Hakuna maoni:
Chapisha Maoni